Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile
Denis Nkane

@denisnkane

ID: 1456211244541698053

calendar_today04-11-2021 10:46:42

82 Tweet

4,4K Followers

7 Following

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Wakati mwingine piga goti mbele za Mungu na mwambie asante, Sio kila siku unapeleka shida zako, wakati wewe unalalamika huna kiatu cha kuvaa kuna watu hawana miguu na wanamshukuru.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Mti ni mmoja ila kila mtu ataona kwa jicho lake,wapo watakao ona ni sehemu ya kupata mbao,wengine wataona watunze ili kupata kivuli,ivyo ndo watu wanakua na mitazamo tofauti juu yako,wapo watakao kudharau ila unatakiwa ubaki kama ulivyo maana familia yako inakutazama kama shujaa

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Kuwa makini na watu unao wachukia. Kuna ndoto haziwezi kutimia mpaka watu wengine watimize ndoto zao kwanza ,usinune wenzio wakifanikiwa pengine furushi la mafanikio yako wamebebeshwa wao, TAFAKARI kuna wafanya kazi wangapapi wa bakhresa wanamafanikio kupitia bakhresa.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Yanapotokea mafuriko Samaki huwala wadudu lakini maji yanapo kauka wadudu huwala samaki. TAFAKARI siku zote Mungu hutoa fursa kwa kila mmoja, isubiri tu zamu yako.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Ex: mtoto anataka kuongea na wewe Mie: Mpe simu Mtoto: tati mgtrsytrrrrrrrrrr Mie: anasema nini..?!! Ex: ety turudianeee❤️❤️😂😂

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Maji ya kunywa ya uhai chupa ndogo maduka ya mtaani yanauza 300. Maji hayo hayo ukienda supermarket yanauzwa adi 1500. Maji hayo hayo pia ukiwa ndani ya airport yanauzwa adi 10000. TAFAKARI kuna mahali wanaweza wasione thamani yako ila kuna mahali utafika wewe ni wa thamani.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Na ukifanikiwa kabla yetu usituone sisi wavivu, wewe shukuru tu sisi pia tunajituma na tunafanya bidii sana nivile baraka zimetangulia kukufikia na sie tupo kwenye mstari zamu yetu itafika

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Dalili moja wapo ya kuonesha Mti unaelekea kustawi hua unaangusha majani yaliyo kauka. Ivyo ndivyo Mungu akitaka kuleta watu bora maishani mwako anaanza na kuwaondoa wasio kufaa.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Sheli wakati inajengwa kitu muhimu cha kwanza hua panazungushiwa fensi ya mabati lengo ni kuficha hatua za ujenzi. Iyo ndo hatua ya kwanza kwenye maisha wakati unatafuta mafanikio hakikisha watu hawajui unafanya nini.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Mwamvuli hauwezi kuzuia mvua kunyesha ila ni vizuri uwe nao utakusaidia kupita kwenye mvua. ivyo ndivyo ujasiri pekeyake hauwezi kukupa mafanikio ila ni vizuri ukiwa nao utakusaidia kupita kwenye changamoto.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Si wamekutupa na kukudharau usiogope. Kuna miembe kibao ipo imestawi njiani kwasababu tu kuna Mtu alikula embe akamaliza akatupa kokwa kama uchafu ila ukachipua muembe.

Denis Nkane (@denisnkane) 's Twitter Profile Photo

Ukifanikiwa kabla yetu sisi usiache kutupokelea simu. Wakati mwengine sio kila simu tunataka kukueleza shida zetu. Kuna muda tunataka kukuambia tupo nyuma yako tunakuombea uzidi kupambana maaana uku mtaani pagumu.