profile-img
Ida Hadjivayanis

@IdaHadjivayanis

Senior Lecturer in Swahili @SOAS Interest in #Africa #Africadiaspora #Education #Translation #Languages #swahiliatsoas

calendar_today16-12-2010 16:53:38

8,6K Tweets

3,6K Followers

562 Following

Ida Hadjivayanis(@IdaHadjivayanis) 's Twitter Profile Photo

Shairi hili limenitoa chozi. Asante sana Komredi wangu, Issa Shivji

Kwa Kamaradi Wangu Chipukizi

Ida mwanangu
Pokea salamu na pongezi zangu.
Nimeshuhudia ukuaji wako kama binadamu,
Kipenzi cha Hawa zaidi ya Adamu.

Sijui kwa bahati au heshima,
Hapana, sio bahati wala heshima

account_circle
Ida Hadjivayanis(@IdaHadjivayanis) 's Twitter Profile Photo

Georgios na mimi tulikupokea ukuingia duniani,
Bila kupiga hodi wala mbwembwe za ughaibuni.

Nimesema sio kwa bahati wala heshima,
Ni tunda la uhusiano wangu na Baba Ida.
Sio wa damu wala kindugu,
Lakini zaidi ya udugu,
Ni uhusiano wa fikra, itikadi na ukamaradi.

account_circle
Ida Hadjivayanis(@IdaHadjivayanis) 's Twitter Profile Photo

Kwa furaha na matumaini,
Nashudia wako ustahili,
Wa msomi na mhadhiri.
Bila ujeuri na kiburi,
Cha msomi mnafiki.

Uendelee na wako unyeyekevu,
Kuhudumia yako jamii kwa wako upevu.
Nakutakia kila la kheri,
Daima uepukane na hulka ijengayo shari.

account_circle