Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profileg
Samia Suluhu

@SuluhuSamia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. President of the United Republic of Tanzania

ID:2652554565

calendar_today29-06-2014 07:42:17

1,2K Tweets

1,6M Followers

27 Following

Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

On behalf of the Government and the people of The United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to the 57th Prime Minister of United Kingdom, Rishi Sunak I’m looking forward to taking our bilateral ties to greater heights. Karibu Tanzania.

On behalf of the Government and the people of The United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations to the 57th Prime Minister of United Kingdom, @RishiSunak I’m looking forward to taking our bilateral ties to greater heights. Karibu Tanzania.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa China Xi Jinping, kwa kuchaguliwa tena kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Heartfelt congratulations to His Excellency President Xi Jinping on being re-elected General Secretary of the Communist Party of China Central Committee.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nawapongeza wanangu Ibrahim na Fadi (Ramadhan Brothers) kwa kipaji na ubunifu wenu wa kucheza sarakasi. Onesho lenu kupitia kipindi Australia's Got Talent limeitangaza vyema nchi yetu ya Tanzania na nawatakia kheri katika kuendeleza sanaa yenu na kushiriki katika maonesho mbalimbali.

Nawapongeza wanangu Ibrahim na Fadi (Ramadhan Brothers) kwa kipaji na ubunifu wenu wa kucheza sarakasi. Onesho lenu kupitia kipindi @GotTalentAU limeitangaza vyema nchi yetu ya Tanzania na nawatakia kheri katika kuendeleza sanaa yenu na kushiriki katika maonesho mbalimbali.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Mmenifurahisha sana Watoto wangu SERENGETI GIRLS kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India. Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali.

Mmenifurahisha sana Watoto wangu @serengetigirls kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India. Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Tumeyazima rasmi majenereta yaliyokuwa yakizalisha umeme Kigoma tangu uhuru, na kuuingiza mkoa katika Gridi ya Taifa. Zaidi ya wananchi 10,000 wa mkoa huu sasa wana umeme wa uhakika. Shughuli za kuleta maendeleo kwenye nchi ni hatua. Kazi Inaendelea.

Kongole Simba Sports Club kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata.

Kongole @SimbaSCTanzania kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nimefurahishwa na ushindi wa tuzo wa mara ya 4 mfululizo wa hifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti kuwa hifadhi bora Barani Afrika. Nawapongeza wadau wote wanaoshiriki katika uhifadhi hapa nchini na nawaomba wananchi tuendelee kuunga mkono uhifadhi ili kukuza uchumi kupitia utalii.

Hongereni Vijana wangu SERENGETI GIRLS kwa ushindi wa 2-1 mlioupata leo dhidi ya Ufaransa. Nawaomba Watanzania tuendelee kuwaombea na kuwatia hamasa vijana wetu ili waendelee kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 huko India.

Hongereni Vijana wangu @serengetigirls kwa ushindi wa 2-1 mlioupata leo dhidi ya Ufaransa. Nawaomba Watanzania tuendelee kuwaombea na kuwatia hamasa vijana wetu ili waendelee kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 huko India.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Mussa Hassan Mussa, Mbunge wa Jimbo la Amani (CCM), Zanzibar. Natuma salamu za pole kwa Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, familia na wakaazi wa Jimbo la Amani. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema Peponi, Amina.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Maulid un-Nabi. Sherehe hii ya kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) iwe tafakari njema tunapoendelea kufanya kazi kuijenga nchi yetu na watu wake, na kuitunza amani, umoja na mshikamano tulio nao.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Leo tunaadhimisha Siku ya Walimu Duniani. Nawatakia kheri ya siku hii walimu wote. Umuhimu wenu katika ujenzi wa Taifa ni wa thamani kubwa. Ahadi yangu ambayo kama Serikali tunaendelea kuitekeleza ni kuhakikisha maslahi yenu yanazidi kuimariki, na kuakisi mchango wenu adhimu.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mtihani wa darasa la saba leo. Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema ili mfanye vizuri mitihani yenu. Serikali itahakikisha maandalizi ya miundombinu ya kuwapokea wote watakaoendelea na kidato cha kwanza mwakani 2023 inakamilika.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Msisitizo wangu kwa Mawakili wa Serikali, Mahakama na taasisi mbalimbali za haki na sheria; mmekabidhiwa sekta ya haki. Haki na mfanya haki ni Mungu peke yake lakini duniani suala la kusimamia haki liko mikononi mwenu. Nendeni kafanyeni uadilifu. Haki isimamiwe. Haki ifanyike.

Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Paul Rupia. Tumeondokewa na mtu aliyetoa mchango mkubwa katika masuala ya kidiplomasia, mageuzi ya kiuchumi na utumishi wa umma, na aliyeweka mbele maslahi ya Taifa. Mungu amweke mahali pema. Amina.

Tunaendelea kutekeleza Mpango wa Elimu bila Malipo kwa kufuta ada ya mitihani ya Kidato cha 4 & 6, ahueni kwa watahiniwa zaidi ya 300,000/mwaka, wengi toka familia zenye kipato kidogo.

Hii inakwenda sambamba na ujenzi wa shule zaidi, maboresho ya mtaala & maslahi ya walimu wetu.

Tunaendelea kutekeleza Mpango wa Elimu bila Malipo kwa kufuta ada ya mitihani ya Kidato cha 4 & 6, ahueni kwa watahiniwa zaidi ya 300,000/mwaka, wengi toka familia zenye kipato kidogo. Hii inakwenda sambamba na ujenzi wa shule zaidi, maboresho ya mtaala & maslahi ya walimu wetu.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bi. Fatma Omar Latu pamoja na dereva wake kilichotokea tarehe 14 Septemba kwa ajali ya gari mkoani Mbeya. Mungu azilaze roho zao mahala pema Peponi. Amin.

account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nimefurahi kushiriki sherehe za uapisho wa Rais wa 5 wa Kenya Mhe. William Samoei Ruto, PhD. Nampongeza Mhe. Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kumaliza uongozi wake na nawapongeza Wakenya wote kwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi kwa amani. Tuendelee kushirikiana kuijenga Afrika Mashariki.

Nimefurahi kushiriki sherehe za uapisho wa Rais wa 5 wa Kenya Mhe. @WilliamsRuto. Nampongeza Mhe. Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kumaliza uongozi wake na nawapongeza Wakenya wote kwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi kwa amani. Tuendelee kushirikiana kuijenga Afrika Mashariki.
account_circle
Samia Suluhu(@SuluhuSamia) 's Twitter Profile Photo

Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa Familia ya Kifalme The Royal Family na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu.

Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa Familia ya Kifalme @RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu.
account_circle